VIKOSI VYA CHINA VYAINGIA INDIA

Indian soldiers at Bumla pass at the India-China border in Arunachal Pradesh. (file photo)
Askari wa India wakiwa kwenye eneo la mpaka baina ya India na China huko Arunachal Pradesh.




India imeituhumu China kupeleka askari katika eneo la magharibi mwa mkoa wa Ladakh katika jimbo la Kashmiri linalotawaliwa na India.



Kwa mujibu wa shirika la habari la Press Trust of India (PTI), waziri wa Ulinzi wa India, Shashikant Sharma na maafisi wengine wa kijeshi walisema katika ripoti iliyowasilishwa mbele ya kamati ya bunge hapo jana Ijumaa, kuwa askari wa China waliingia umbali wa kilometa 19 ndani ya ardhi ya India Aprili 15. 



Aidha, waziri huyo wa ulinzi aliwaambia wabunge waliohuduhuria katika kikao hicho kuwa India imepeleka askari katika eneo hilo lenye mzozo ili "kuulinda mpaka huo."



"Maafisa hao waliiambia kamati hiyo kuwa Aprili 16 askari wa India walitoa taarifa ya kuwepo kwa wanajeshi wa China walioweka kambi kilometa 19 ndani ya eneo lijulikanalo kama LAC (Line Actual Contol)." 



LAC ni eneo la mpaka linalogombaniwa baina ya China na India linalopita katika milima ya Himalayas.



Mnamo siku ya Alkhamisi, Waziri wa mambo ya nje wa India, Salman Khurshid alisema kuwa ataelekea nchini China tarehe 8 Mei, akisema kuwa India na China zina makubaliano ya pamoja ya kutoruhusu mzozo huo "kuharibu" uhusiano wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.



Wakati huo huo, siku ya Ijumaa, afisa wa Wizara ya Mambo ya nje ya India alisema kuwa Waziri Mkuu wa China Li Keqiang angeitembelea India baadaye mwezi Mei.



Mpaka sasa mazungumzo baina ya nchi hizo mbili yameshindwa kutatua mzozo wa eneo la magharibi la mkoa wa Ladakh katika jimbo la Kashmir.



Maafisa wa India wanadai kuwa Aprili 15 kikosi cha jeshi la China kiliweka kambi ndani ya ardhi ya India.



India iliwataka askari wa China kuondoka, lakini vikao kadhaa baina ya makamanda wa kijeshi wa eneo hilo na wanadiplomasia kutoka pande zote mbili vimeshindwa kutanzua mzozo huo. China imekanusha kufanya kosa lolote.



India na China zimekuwa na uhusiano usioridhisha tangu mwaka 1962, zilipopigana katika mikoa ya Ladakh na Arunachal Pradesh iliyopo katika eneo la milima ya Himalaya. 

China inadai kilometa za mraba 90,000 za ardhi ya Arunachal Pradesh, lakini India inasema kuwa China imevamia kilometa za mraba 38,000 za eneo la India la uwanda wa Aksai Chin. 

India na China zimewahi kufanya mazungumzo mara 15 ili kutanzua mgogoro wa mpaka baina yao tangu mwaka 1962 lakini suala hilo limeshindikana kutatuliwa.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment