UJERUMANI: RAIS WA ZAMANI ASHITAKIWA KWA UFISADI

Former German President Christian Wulff
Rais wa zamani wa Ujerumani President Christian Wulff



Rais wa zamani wa Ujerumani, Christian Wulff ameshitakiwa kwa kosa la kupokea hongo kwa maslahi na manufaa ya kisiasa.


Mwendesha mashitaka katika mji wa kaskazini wa Hanover aliwasilisha mashitaka ya ufisadi dhidi ya Wullf kwa tuhuma za upendeleo zilizomlazimu kujiuzulu mwaka jana.


Waendesha mashitaka wanamtuhumu Wulff kwa kuishawishi kampuni ya Siemens AG kusaidia kuuza filamu ya “John Rabe”, baada ya mtengeza filamu mmoja kumlipa rais huyo wa zamani kiasi cha yuro 4,000 kugharamia safari yake na familia yake wakati alipotembelea tamasha la Oktoberfest la mjini Munich mwaka 2008. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Aprili 9 Wullf kukataa ofa ya nyumba na malipo yatokanayo na kuwa mtumishi wa umma yanayofikia yuro  50,000 ($65,000), akisema kuwa bora apambane  mahakamani ili kusafisha jina lake.


Wulff alijiuzulu mnamo Februari 2012, baada ya waendesha mashitaka kuliomba bunge kuondosha kinga ya kutoshitakiwa baada ya kumshuku na kumtuhumu kuwa alipokea hongo alipokuwa gavana wa Saxony.  

Kashfa hizo ziliibuliwa na gazeti la Kijerumani la Bild, likimtuhumu kulipotosha bunge kuhusu mkopo wa nyumba ya bei chee aliouchukua kutoka kwa rafiki yake mmoja mfanyabiashara.



Baaadaye Wullf aliomba radhi hadharani kwa kumtishia mhariri wa gazeti hilo kwa "vita" kama habari hiyo ingechapishwa.

Kama Wulff atafika mahakamani kujibu mashitaka hayo, atakuwa rais mstaafu wa kwanza wa Ujerumani kufanya hivyo.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment