MAKAHABA 35 WAKAMATWA KINONDONI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Charles Kenyela

Jeshi la polisi mkoa wa kinondoni limetangaza vita maalum ya kuwasaka madada poa , msako huo utahusisha nyumba hadi nyumba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, aliviambia vyombo vya habari kuwa, tayari wameshaanza msako huo katika operesheni maalum iliyoanza hivi karibuni.

Amesema mbali na makahaba hao pia wamekusudia vilevile kuwakamata wamiliki wa nyumba zinazojihusisha na biashara hizo.

Amesema wamiliki wa nyumba hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria kujihusisha na biashara hizo hata kama akibainika kumpangisha mpangaji yeyote anayejihusisha na kuuza mwili wake.





Amesema jeshi hilo limejipanga vilivyo kukabiliana na biashara hiyo ambayo inasababisha ongezeko la maambuzi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Amesema katika operesheni hiyo tayari wameshaweza kuwakamata makahaba zaidi ya 35 waliokamatwa maeneo tofauti ya Kinondoni.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment