NDEGE ZA ISRAELI ZAUSHAMBULIA UKANDA WA GAZA



Smoke rises after an Israeli airstrike on Gaza City, November 21, 2012.
Moshi mzito baada ya mashambulizi ya ndege za Israeli kwenye mji wa Gaza, Novemba  21, 2012.

Ndege za kivita za Israeli zimefanya mashambulizi matatu kwenye eneo la Ukanda wa Gaza.



Mashuhuda wa Kipalestina wanasema kuwa ndege za Israel ziliyashambulia kwa mabomu mazito maeneo mbalimbali ya mji wa kusini wa Khan Younis na jirani na mji wa Rafah kusini mwa Gaza alfajiri ya leo.


Hakuna maafa yaliyoripotiwa. Na jeshi la Israeli limethibitisha kufanya mashambulizi hayo.


Mapema mwezi Aprili, Israeli ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa mara ya kwanza tokea kufikiwa makubaliano yaliyohitimisha vita ya siku nane ya Israeli dhidi ya ardhi za Palestina mwezi Novemba 2012.



Katika mashambulizi hayo yaliyoanza Novemba 14 mpaka 21, zaidi ya Wapalestina 160, wakiwemo wanawake na watoto, walipoteza maisha yao na zaidi ya 1200 kujeruhiwa.



Gaza imekuwa katika mzingiro uliowekwa na utawala wa Israeli tangu Juni 2007, hali ambayo imesababisha mazingira magumu ya maisha kwa wakazi wa eneo hilo.



Israel inawanyima watu wapatao milioni 1.7 wa Gaza haki zao za msingi, kama vile huduma muafaka za afya na elimu.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment