MALI: WAKIMBIZI 74,000 WANA HALI MBAYA



A Malian refugee girl pulls water at the Mbere refugee camp in southern Mauritania. (File photo)
Binti mkimbizi kutoka Mali akivuta dumu la maji katika kambi ya wakimbizi ya Mbere kusini mwa Mauritania.



Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linasema kuwa raia 74,000 kutoka Mali waliokimbilia katika jangwa la Mauritania wanahitaji msaada wa haraka.


Shirika hilo lijulikanalo pia kama Medecins Sans Frontieres, linasema kuwa hali ya wakimbizi hao katika kambi ya Mbera ni ya kutisha na kwamba "misaada ya kibinaadamu haitoshi."


Vilevile, MSF inasema kuwa wakimbizi hao wanapata shida ya ukosefu wa huduma za msingi na usalama wa chakula ni wa kusikitisha. Pia kuna ukosefu wa maji katika kambi hiyo, huku hali ya joto ikipinda kwa nyuzi 50.
 

Afisa wa misaada ya dharura wa MFS, Marie-Christine Ferir anasema kuwa watoto wanalazimika kupata mgao wa "maziwa yenye virutubisho maalumu ili kuepuka utapiamlo."

 

Aidha, Ferir anasema kuwa kiwango cha vifo vya watoto katika kambi hiyo kimeongezeka. "Kwa sasa kiwango kimezidi kiwango cha dharura cha vifo viwili kwa watu 10,000 kwa siku. Sasa kiwango kimefikia 3.2 kwa watu 10,000 kwa siku."



Kwa mujibu wa Ferir, watoto 23 mpaka 24 hufariki kwa wasitani wa kila siku katika kambi hiyo ya Mbera. 

Vita ya Mali, iliyoanzishwa na Ufaransa mnamo Januari 11, imesababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo na kuwahamisha maelfu ya watu ambao sasa wanaishi katika hali mbaya na ya kusikitisha.


Mnamo Februari 27, John Ging, mkurugenzi wa operesheni wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Misaada na Huduma za Kibinaadamu, alisema watoto wa Mali wapatao 200,000 hawapati elimu yoyote.


Pia mnamo Februari 1 shirika la Amnesty International lilisema kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinaadamu katika vita hiyo - ikiwa ni pamoja na mauaji ya watoto.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment