IRAQ: 12 WAUAWA, 30 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO WA BOMU

Firefighters and people gather at the site of an explosion near a mosque in Baghdad. (File Photo)
askari wa zimamoto na wananchi wa kawaida wakiwa wamekusanyika katika eneo la tukio mjini Baghdad.




Kwa uchache watu kumi na mbili wameuawa na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu jirani na msikiti kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.


Mlipuko huo ulitokea wakati waumini wakiondoka katika msikiti wa Omar bin Abdul Aziz katika mji wa Kanaan, takriban kilometa 75 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, baada ya Swala ya Ijumaa.


Shirika la habari la AP limeripoti kuwa, dakika chache baada ya shambulizi la Kanaan, bomu jingine liliripuka jirani na msikiti wa wafuasi wa madhehebu ya Shia magharibi mwa Baghdad na kujeruhi watu 8.


Mashambulizi haya yanakuja kabla ya uchaguzi wa majimbo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Mnano Aprili 20 katika majimbo 12 kati ya majimbo 18 ya Iraq. 



Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mwezi uliopita watu 271 waliuawa, ikiwa ndiyo idadi kubwa kabisa ya vifo kwa mwezi tangu Agosti mwaka jana.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment