MIMBA MILIONI 336 ZACHOMOLEWA NCHINI CHINA NDANI YA MIAKA 40




SERA ya China ya kuzaa mtoto mmoja tu imeibua mjadala mzito kuhusu matokeo na athari zake kiuchumi kutokana na umri wa raia wake.

kwa mujibu wa data rasmi kutoka wizara ya afya ya nchi hiyo, madaktari nchini humo wamechomoa zaidi ya mimba milioni 330 tangu serikali ilipoanza kutekeleza sera tata ya kuzaa mtoto mmoja miaka 40 iliyopita.

Taarifa zilizowekwa kwenye tovuti ya wizara ya afya zinaonesha kuwa tangu mwaka 1971 – muda mfupi kabla ya China kuanza kuhamasisha watu kuzaa watoto wachache – madaktari wamechomoa mimba milioni 336.

Awali serikali ya China ilikadiria kwamba bila kuweka sera ya ukomo wa kuzaa, idadi ya raia wa nchi hiyo ambao ni bilioni 1.3 ingeongezeka kwa asilimia 30.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa mbali na uchomoaji wa mimba, tangu mwaka 1971 madaktari wamewahasi wanaume na wanawake milioni 196.
Uongozi mpya wa China umeshachukua hatua ya kuvunja Tume ya Uzazi wa Mpango.

““Baada ya mageuzi hayo, China italazimika kutekeleza na kuboresha sera ya uzazi wa mpango,” Shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua, lilimnukuu katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Ma Kai, alisema wakati hatua hiyo ilipotangazwa siku ya Jumamosi.

Hatua hiyo ilijumuishwa katika ripoti kuhusu muundo mpya wa serikali iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo, ambacho kilimaliza mkutano wake wa mwaka hapo jana Jumapili.

China imetangaza mabadiliko ya kimuundo kwenye mfumo wake wa uzazi wa mpango ambao hufuatailia na kusimamia sera ya mtoto mmoja wakati wa mkutano huo uliofanyika mjini Beijing.

China inasema kuwa sera yake hiyo imezuia ongezeko mara dufu la watu na kuimarsiah uchumi wake.

Sera hiyo, ambayo inataka wale wanaoishi mjini wazao mtoto mmoja tu, na kutoa tahfifu  kwa familia za vijijni. Wale wanaokiuka sheria hiyo wanatakiwa kulipa faini.
Hata hivyo, wito umeengezeka kutaka sheria hiyo iondolewa kwa kuwa nguvu kazi ya taifa inayumba na tabaka la wazee linaongezeka. Makundi ya haki za binaadamu yamekosoa “njia kali katika utekelezaji wa sheria hiyo”.

Jumapili iliyopita, serikali ilitangaza Tume ya Ongezeko la watu na ile ya Uzazi wa mpango zimeunganishwa pamoja na wizara ya afya katika hatua ambayo vyombo vya habari vya serikali vinasema inakusudia kuiboresha sera ya mtoto mmoja na sio kuiondosha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua, sensa ya mwaka 2010 nchini China, inaonesha kuwa raia wa nchi hiyo wangeongezeka kwa milioni 400 zaidi kama sera ya mtoto mmoja isingetekelezwa.

CHANZO: MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment