MBUNGE AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Chambani (CUF) Salim Hemed Khamis



Mbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis amefariki dunia. Mbunge huyo alianguka jana ghafla akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake.
Mbunge huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya afya yake amefikwa hali hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward Lowasa jana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuanguka ghalfa.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment