| Naibu Mkurugenzi wa Bodi ya Uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Kenya, Henry Ochido (kushoto), akiwa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi Desemba 16, 2014, ambapo alieleza kuwa mashirika 15 yamefutiwa usajili kwa tuhuma za kufadhili shghuli za kigaidi. |
Serikali nchini Kenya imeyafunga zaidi ya mashirika (NGOs)
500, baadhi yake yakituhumiwa kufadhili ugaidi.
Naibu mkurugenzi wa Bodi ya Kuratibu mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali, Henry Ochido, amesema kuwa jumla ya mashirika 15 kati
ya 537 hayo, akunti zake zimefungwa na taarifa zake kupelekwa kwenye idara za
usalama kwa kuhusishwa na ugaidi.
“Baadhi ya mashirika yamekuwa na yameendelea kutumika
katika vitendo vya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kufadhili ugaidi nchini Kenya na
katika eneo la Pembe ya Afrika,” ilisema taarifa ya bodi hiyo.
Orodha hiyo inajumuisha mashirika 510 – yakiwemo makundi
ya uwezeshaji kwa wanawake, mashirika ya maendeleo vijijini na makundi ya
kusaidia watu wanaioshi na virusi vya Ukimwi- ambayo yamedaiwa kukiuka sheria
ya masharika yasiyokuwa ya kiserikali nchini humo na kushindwa kujibu taarifa
ya kusudio la kufutwa kwa vyeti vya usajili wao.
Mashirika mengine 12, ikiwa ni pamoja na shirika la
Madaktari wasiokuwa na Mipaka (Medecins Sans Frontieres) na Concern Worldwide, yanatarajiwa
kufutiwa usajili kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha ripoti za mahesabu yake.
Mamia ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yapo hatarini
kufutiwa usajili ndani ya kipindi cha wiki tatu zijazo, amesema Ochido.
Wataalamu wameikosoa sheria ya mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali ya mwaka 1990 kuwa ni yenye kasoro nyingi, ambapo huifanya serikali
kuyaingilia mashirika hayo na kuyanyima uhuru wa kujiendesha.
Kwa sasa Kenya ina zaidi ya askari 3,000 kusini mwa
Somalia, ambapo wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa al-Shabab. Uamuzi huo
ulichukuliwa mwaka 2011, baada ya kundi hilo kudaiwa kufanya mashambulizi
kadhaa ndani ya Kenya.
Kundi hilo limekuwa likidai kuhusika na mashambulizi
mbalimbali nchini Kenya, likisema kuwa linalipiza kisasi dhidi ya uwepo wa
maelfu ya askari wa Kenya nchi Somalia ambao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa
Afrika kinachoisaidia serikali ya Mogadishu.
0 comments:
Post a Comment