BEIJING — Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 limepiga
katika eneo la jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China na kusababisha kifo
cha mtu mmoja, shirika la habari la nchi hiyo Xinhua limeripoti.
Tetemeko hilo limepiga umbali wa kilometa 40 kutoka mji
wa Kangding kwenye kina cha kilometa 18, kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha
Matetemeko cha nchi hiyo.
Majengo yanaripotiwa kutikisika sana na mwanamke mmoja
kikongwe kufa baada ya kupigwa na kioo kilichovunjika.
Wakazi wa mji mkuu wa jimbo hilo, Chengdu, waliathiriwa
na tetemeko hilo.
Matetemeko ya ardhi hulipa mara kwa mara eneo la kusini
magharibi mwa China. Mwaka 2008 tetemeko la ardhi liliua watu wapatao 70,000
katika jimbo hilo la Sichuan.
0 comments:
Post a Comment