Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha
wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa
wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC
zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na
uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi
kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba
inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu
zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio
watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu
zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na
wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa
mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao
2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao
ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba
juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa
kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa
kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza
kutekelezwa msimu huu
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni
zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia
Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji
watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu
utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu
Twite na uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni
zipi zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni
na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea
timu ya Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam
FC pia alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013,
alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni
kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka
siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea
kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki
wa Young Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa kuwa
wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka,
hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana
hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao
pamoja na ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa
hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana
mipango ya msimu ujao.
Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake,
wapenzi na washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao
kwani Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea
kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika
usajli wa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment