Wafanyakazi wanaojenga uwanja wa Olympic
mjini Rio de Janeiro, wametangaza kuendelea mgomo wa kutofanya kazi, licha ya
kamati ya Olympic ya kimataifa IOC kutarajia kutembelea uwanjani hapo kujionea
maendeleo ya uwanja huo katika siku chache zijazo.
Wafanyakazi karibu 2500, ambao wamekusanyika
nje ya uwanja huo ambao utashuhudia michezo yote ya Olympic ikichezwa mwaka
2016, wametangaza msisitizo huo kutokana na ujira kidogo wanaolipwa.
Raisi wa umoja wa wafanyakazi hao Antonio Figueiredo Souza, amesema mpaka sasa hawajaelewa ni lini watafanya maamuzi ya kurejea kazini, kutokana na malalamiko yao kuwasilishwa kwenye mahakama ya kazi ambapo wanaamini ndipo haki yao itapatikana.
"Hatutarajii kurejea kazini hata kama kamati ya Olympic ya kimataifa IOC itatembelea kwenye uwanja Olympic Park, na suala hilo halitutishi kutokanana kuzitambua haki zetu ambazo tunastahili kulipwa” Amesema Antonio Figueiredo Souza.
Mgomo wa wafanyakazi hao ulianza tangu April 3 mwaka huu, na wamekua wakifika uwanjani hapo na kujikusanya kwa makundi kwa lengo la kujadilina masuala muhimu, ambayo wanaamini yatawasaidia katika kudai haki zao.
Hata hivyo imeelezwa kwamba mgomo wa wafanyakazi hao unaendelea kuathiri mipango ya ujenzi wa uwanja wa Olympic Park, hali ambayo huenda ikasababisha uwanja huo kumalizika nje ya muda uliokuwa umekusudiwa.
Kama itakumbukwa vyema tatizo la mgomo pia limeathiri maandalizi ya fainali za kombe la dunia ambayo yameshindwa kukamilika kwa wakati, hatua ambayo imepelekea ujenzi wa baadhi ya viwanja kushindwa kukamilika kwa wakati mpaka hivi sasa, ambapo imesalia miezi miwili kabla ya kuanza kwa fainali hizo.
Nchi ya Brazil itakua mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 na kisha mwaka 2016 itakua mwenyeji wa michuano ya Olympic katika jiji la Rio de Janeiro.
0 comments:
Post a Comment