Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki |
MAFURIKO yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa
wiki yamesababisha vifo vya watu 41.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema
vifo 25 vimethibitishwa. Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu
wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea
vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani. Kinondoni vifo ni
saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke
vifo saba.
Sadiki alitaka uchunguzi wa polisi ufanyike kila familia
zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo 14
vilitokana na mafuriko.
Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani
alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.
Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani
inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi
yake.
CHANZO: Habari Leo
0 comments:
Post a Comment