Pichani juu ni baadhi ya wanafunzi wasioona wakitumia vifaa maalum kwa ajili kuandikia maandishi yenye nundu ambayo husomeka kwa njia ya kupapasa. Kalamu ya kuandikia huwa na ncha kali kama sindano ya fundi. Karatasi za kuandikia huwa ngumu kuweza kutoa vinundu ambavyo husomeka kwa kupapaswa.
Mwenyekiti wa Kundi la akinamama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. S. Mwasilu akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Msingi Wasioona ya Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara msaada wa magodoro na zawadi mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. S. Mwasilu na Katibu wake Bi. Joyce Mwanandenje wakigawa zawadi za biskuti kwa wanafunzi wasioona wa Shule ya Msingi Malangali katika hafla fupi ya kutoa msaada shuleni hapo. Picha ya juu ni sehemu ya Msaada uliotolewa shuleni hapo.
Katibu wa kundi la akinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. Joyce Mwanandenje akizungumza kwa niaba ya umoja huo ambapo alisema lengo la ujio wao Shuleni hapo ni kutimiza desturi yao ya kila mwaka ambapo hutembelea makundi ya wahitaji mbalimbali katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani. Katika salam zao shuleni hapo walitoa msaada wa magodoro 20, Sukari, sabubi na zawadi mbalimbali kwa aijili ya wanafunzi. Kundi hila la akinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa linaundwa na watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hazina Ndogo, Ukaguzi wa Ndani, Chuo Kikuu Huria na Baraza la Nyumba na Ardhi Mkoa.
Picha ya Pamoja kati ya uongozi wa shule ya wasioona Malangali, na kundi la akinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment