RIPOTI: NDANI YA KILA SAA 1 MATUKIO 3 YA UBAKAJI HUTOKEA KATIKA JESHI LA MAREKANI

Many victims fail to report sexual assault out of fear of vengeance or lack of justice under the US military’s system of prosecution.
waathirika wengi hushindwa kutoa taarifa kwa kuhofia kisasi au ukosefu wa haki chini ya mfumo wa mashitaka wa kijeshi.


RIPOTI mpya iliyotolewa na Idara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, inasema kuwa takriban matukio matatu ya ubakaji hutokea ndani ya kila saa moja katika jeshi la nchi hiyo, na hivyo kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu kiwango cha matukio ya dhulma za kingono kwa askari wake.



Siku ya Jumanne, gazeti la  Washington Post  lilisema kuwa kwa mujibu wa Pentagon, matukio ya unyanyasaji wa kingono jeshini yameongezeka mpaka kufikia kiwango cha hatari kwa matukio 70 kwa siku au matatu ndani ya saa moja.  

Ripoti hiyo iliongeza kusema kuwa askari wapatao 26,000 walikumbwa na mkasa huo kwa mwaka 2012, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35 tangu mwaka 2010 iliporipotiwa mikasa  19,000.  

Hata hivyo, ripoti inaongezea kusema kuwa, kuna uwezekano kuwa kiwango cha visa vya dhulma za kingono katika jeshi la Marekani ni kikubwa zaidi, kwa kuwa waathirika wengi hushindwa kutoa taarifa kwa kuhofia kisasi au ukosefu wa haki chini ya mfumo wa mashitaka wa kijeshi.    

“Kadiri  taasisi inavyokosa uwazi na kuwa na msonge wa madaraka, ndivyo waathirika wanavyonyanyapaliwa na wabakaji kuzoea," alisema Susan Brooks, pasta na mshauri wa mikasa ya ubakaji.



Brooks alienda mbali zaidi na kulilaumu jeshi la Marekani kwa kufuga utamaduni wa uhusiano wa jinsia na mamlaka, ambao anasema unazalisha utamaduni wa ubakaji miongoni mwa askari.


Kwa miaka mingi, makamanda wengi wa ngazi za juu katika jeshi la Marekani wamekuwa wakitiwa hatiani na kuachishwa kazi kutokana na makosa mengi ya udhalilishaji wa kingono.


Mnamo Mei 6, mamlaka zilisema kuwa Luteni Kanali Jeff Krusinski, mkurugenzi wa programu ya kuzuia hujuma za kingono katika jeshi la Anga la Marekani, yeye mwenyewe aliwekwa kizuizini kwa kumdhalilisha kingono mwanamke mmoja nje kidogo ya makao makuu ya jeshi hilo Arlington, Virginia. 

Mwaka 2012, zaidi ya wakufunzi wa 30 wa kiume katika kambi ya jeshi la Anga walitiwa hatiani kwa kuwabughudhi, kuwadhalilisha na kuwabaka makuruta wapatao 59 katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Lackland, Texas. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment