Prof Lipumba awalaumu watawala kwa uchumi mbovu nchini

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema uchumi wa Tanzania umekuwa ukiporomoka siku hadi siku kutokana usimamizi mbovu wa watawala. Profesa Lipumba alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont katika mkutano wa wadau wa maendeleo.

Mkutano huo uliandaliwa na CUF kwa kushirikiana na chama rafiki cha Redikale Venstre cha Denmark.

Alisema Tanzania ina raslimali za kutosha ambazo zinaweza kuondoa umaskini wa wananchi.

Hata hiyo, alisema raslimali hizo zimekuwa zikiwanufaisha zaidi wageni.

Profesa Lipumba alisema Serikali inapaswa kuwabana wawekezaji katika sekta ya madini waweze kulipa fedha za kutosha kutokana na raslimali wanazovuna badala ya kutegemea kupata mrahaba huku wawekezaji hao wakivuna mamilioni.

“Ili kuwalinda wananchi na raslimali zilizopo mikataba iliyopo imejaa upendeleo kwa wageni unadhani mwananchi wa kawaida na serikali wataambulia nini…watawala wanapaswa kusimamia raslimali kwa kamilifu kwa niaba ya wananchi,” alisema.

Alisema CUF na chama rafiki kutoka Denmark wataendelea kufanya mikutano katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuzungumza na wananchi kujua faida ya raslimali zinazopatikana katika maeneo yao.

“Kikao cha leo kama mlivyowasikia wananchi ni kuwa wanalalamika raslimali haziwanufaishi kwa namna yoyote ile.

“Hivyo ni jukumu kwa CUF kuhakikisha wananchi wananufaika na raslimali pia tutaendelea kupiga kelele kwa watawala ili wawajibike kwa ajili ya watanzania na siyo vinginevyo,” alisema Profesa Lipumba.
Chanzo:Mtanzania
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment