KIMBUNGA CHAUA DAZENI YA WATU NCHINI MAREKANI



Teachers carry children away from Briarwood Elementary School after a tornado destroyed the school in south Oklahoma City on May 20, 2013.
Walimu wakiwahamisha wanafunzi kutoka shule ya awali ya Briarwood baada ya kimbunga kulikumba jimbo la Oklahoma Mei 20, 2013. 



TUFANI nzito imepiga eneo la jimbo la Oklahoma, kuwaua watu wasiopungua 91, wakiwemo watoto wa shule ya awali na kusababisha uharibifu mkubwa uliotokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi ya maili 200 (kilometa 320) kwa saa. Mamlaka za mji huo zinasema kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.


Kimbunga hicho kilichopiga kwenye kiunga cha mji wa Moore jumatatu mchana kwa saa za huko, kuvunja nyumba, shule mbili na hospitali, huku watu 120 wakijeruhiwa na wengine kadhaa kuripotiwa kupotea.



Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini humo, mkondo hatari wa kimbunga bado unatoa kitisho kwa majimbo mengine 10 kwa kuwa vimbunga vingi bado vinatarajiwa kutokea.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment