BUNGE LA VENEZUELA LAGEUKA UWANJA WA MASUMBWI




Venezuelan parliamentarians fight in the National Assembly, April 30, 2013.
Wabunge wa Venezuela wakipigana Bungeni jana Aprili 30, 2013.


Vurugu zilizuka ndani ya Bunge la Venezuela baada ya kuibuka kwa mabishano kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais uliomalizika hivi karibuni.


Maipgano hayo yalitokea jana Jumanne baada ya bunge kuchukua hatua ya kikanuni inayowanyima wabunge wa upinzani haki ya kuzungumza bungeni mpaka wautambue ushindi wa Rais Nicolas Maduro wa Aprili 14. 

"Mpaka wazitambue mamlaka, taasisi za umma, mamlaka ya wananchi wetu, wawakilishi wa upinzani itabidi waende kuzungumza na vyombo vya habari (binafsi) sio katika bunge hili," alisema kiongozi wa bunge Diosdado Cabello.

Aidha, wabunge wa chama tawala waliulaumu upinzani kwa kuanzisha mapigano.


"Tulitambua kuwa wapinzani wamekuja kuzusha fujo na ghasia," alisema Maduro baada ya tukio hilo na kuongeza kuwa, "jambo hili halipaswi kujirudia."


Mfanyakazi mmoja wa bunge alisema kuwa tukio hilo lilianza baada ya wabunge wa upinzani kupiga makele kwa nguvu wakisema “fashisti” na kiongozi wa bunge akainua bango lililosomeka “mapinduzi ya bunge.” 

Katika mapigano hayo, watu kadhaa walishambuliwa na kujeruhiwa, akiwemo mbunge wa chama tawala Odalis Monzon. 


"Leo tena nililazimika kuitetea historia ya Kamanda wetu (marehemu Rais Hugo Chavez)," alisema Monzon. 

Kwa upande mwingine, wapinzani wanawalaumu wafuasi wa Maduro kwa tukio hilo, baada ya mbunge mmoja kuonekana kwenye kituo kimoja cha televisheni akionesha majeraha aliyoyapata.

Maduro alimshinda kiongozi wa upinzani Henrique Capriles kwa kupata asilimia 50.7 ya kura dhidi ya asilimia 49.1 za mpinzani wake, tofauti ikiwa ni kura 235,000. 

Capriles alikataa kuutambua ushindi wa Maduro akidai kuwa kuna rafu ilitendeka wakati wa uchaguzi.


Hata hivyo, mnamo Aprili 28, Tume ya Uchaguzi ilisema kuwa Capriles ameshindwa kuleta uthibitisho wa madai ya kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi wa urais.


Leo Mei 1, wafuasi wa chama tawala na wale wa upinzani wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Caracas, kuadhimisha Sikukuu ya Mei Mosi.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment