Vyama vya kisiasa Afrika vyakutana Sudan

Sudanese President Omar al-Bashir gives a speech during the first conference of the Council of the African Political Parties on April 27, 2013 in Khartoum.
Rais Bashir wa Sudan akihutubia mkutano wa vyama vya kisiasa Afrika, Khartoum Aprili 27 2013



Wawakilishi wa vyama 35 vya kisiasa barani Afrika vyenye uwakilishi bungeni wamekutana katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum kwa lengo la kuanzisha jukwaa la kuimarisha umoja wa nchi za Afrika.

Akihutubia kikao hicho cha Baraza la Vyama vya Kisiasa Afrika siku ya Jumamosi, Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema kikao hicho ni hatua ya kwanza ya kimsingi ya kuleta umoja kamili barani Afrika.

Rais Bashir amesema pamoja na kuwa bara la Afrika lina historia iliyojaa utajiri na idadi ya watu wanaozidi bilioni moja, lakini bado Waafrika hawana uwakilishi unaofaa katika vikao vya kimataifa.  Mshauri wa Rais wa Sudan Nafie Ali Nafie amesema kikao hicho kinalenga kuleta umoja na kuunda taasisi ya vyama vyote vya kisiasa Afrika.  Kamishna wa Masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Afrika Bi. Aisha Abdullahi pia alihudhuria sherehe za ufunguzi wa kikao hicho.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment