IRAN: TETEMEKO LA ARDHI LAUA 33 NA KUJERUHI MAMIA




Tetemeko zito la adrdhi lenye ukubwa wa 6.1 kwenye kipimo cha Richter limeupiga mji wa Kaki jirani na jiji la kusini mwa Iran la Bushehr, na kuua watu wapatao 33 na kujeruhi zaidi ya watu 850.


Kwa mujibu wa Kituo cha Seismolojia cha Iran, tetemeko hilo limeupiga mji wa Kaki, kilometa 90 kusini mashariki mwa mji wa Bushehr, leo saa 10:22 kwa saa za nchi hiyo umbali wa kilometa 12 chini ya ardhi.


Tetemeko hilo lilifuatiwa na mishituko 4 iliyoutikisa mji wa Kaki na mji wa jirani wa Khour-Mowj. 

Nchi za Ghuba ya Uajemi za Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu zilishuhudia mishituko iliyotokana na tetemeko hilo.


Kampuni ya Kirusi iliyojenga kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Bushehr ilisema kuwa tetemeko hilo halikuathiri shughuliza kinu hicho.


Kinu hicho kipo kilometa 18 kusini mwa mji wa Bushehr na takriban kilometa 160 kutoka eneo lililopigwa na tetemeko hilo.  

“Tetemeko halikuathiri kwa namna yoyote hali ya kawaida ya kinu cha Nyuklia cha Bushehr. Watu wanaendelea kufanya kazi kama kawaida na kiwango cha mionzi kipo katika hali ya kawaida," alinukuliwa afisa wa kampuni hiyo.



Gavana wa mkoa wa Bushehr naye aliwaambia waandishi wa habari kuwa kinu hicho cha nishati hakikuharibiwa katika tetemeko hilo.


Mwezi wa Desemba 2010, tetemeko kubwa la ardhi liliua watu 31,000 katika mji wa kusini mashariki wa Bam.

CHANZO: Press Tv
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment