AUSTRIA: KASISI WA ZAMANI ASHITAKIWA KWA KUWADHALILISHA WATOTO KIJINSIA

A file photo of Kremsmuenster monastery in northern Austria
Shule ya Kitawa ya Kremsmuenster kaskazini mwa Austria






Waendesha mashitaka nnchi Austria wamemshitaki kasisi wa zamani kwa kuwadhalilisha kijinsia wanafunzi kadhaa kwenye shule moja ya bweni.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa Austria ilisema kuwa Alfons August Mandorfer mwenye umri wa miaka 79 anatuhumiwa kuwadhalilisha kingono watoto 15, kuwatesa na kuwasumbua wanafunzi wengine, alipokuwa mkuu wa shule ya kitawa ya Benedictine kati ya mwaka 1973 na 1993 katika mji wa kaskazini wa  Kremsmuenster.

Mbali na mashitaka hayo, pia kasisi huyo anatuhumiwa kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Habari hiyo ni sehemu ya uchunguzi huru uliofanywa na Kanisa Katoliki la Austria dhidi ya madai ya udhalilishaji wa kingono na aina nyingine za udhalilishaji uliofanywa na viongozi wake.

Uchunguzi huo ulioanza mwaka 2000, mpaka Aprili 2012 umeibua zaidi ya tuhuma 700, baadhi yake zikiwa zilifanyika miaka ya 1960.

Wakati huo huo, mnamo Aprili 6 makasisi watatu wa Kimarekani walisimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo kufuatia tuhuma za dhulma za kingono na mwenendo mbaya dhidi ya watoto.

Kanisa Katoliki limekuwa likikumbwa  na kashfa nyingi huko Marekani na Ulaya kwa miaka kadhaa iliyopita, ikihusisha tuhuma za kufunika dhulma za kingono zilizofanywa dhidi ya watoto ili kuwalinda makasisi na kulinda heshima ya kanisa.

Ripoti zilibaini kuwa zaidi ya makasisi 4,000 wa Marekani walikabiliwa na tuhuma za dhulma za kingono tangu miaka ya 1950, katika kesi na matukio yaliyowahusisha zaidi ya watoto 10,000.

Mnamo Machi 13, Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina alichaguliwa kuwa papa mpya wa Kanisa Katoliki na kuchukua jina la Papa Francis I. Mtandao ujulikanao kama The Survivors Network of Those Abused by Priests (SNAP), ambao ni mtandao wa waathirka wa vitendo hivyo, ulimtaka papa mpya kuiweka vita dhidi ya uhalifu wa kingono uliofanywa na makasisi kuwa ajenda ya kwanza ya Kanisa lake.

IMEANDALIWA NA MZIZIMA 24 KWA MSAADA WA MTANDAO
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment