Baba aua mwanaye, amfukia sebuleni

Na Pendo Fundisha, Mbeya
JESHI la Polisi, mkoani Mbeya, linamshikilia Riziki Mwangoka (27), mkazi wa Iponjola, wilayani Rungwe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtoto wake wa miaka mitatu. Mwanamume huyo anadaiwa kumuua mtoto huyo na kisha maiti yake kuifukia katika shimo alilochimba katika sebule ya nyumba yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alisema tukio hilo lilitokea Februari 27, mwaka huu saa saba mchana katika kijiji hicho.

Kamanda Athumani, alisema mwili wa mtoto huyo, Debora Riziki uligundulika akiwa amepoteza maisha baada ya kufukiwa katika shimo hilo ndani ya nyumba ya baba yake.

Alisema, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Februari 29 mwaka huu na kwamba chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa ndoa baina ya mtuhumiwa na aliyekuwa mke wake, Esther Msafiri (23), mkazi wa Kibumbwe wilayani Rungwe.

Kamanda Diwani alisema kuwa mgogoro huo ulikuwa ni mvutano wa nani anayepaswa kuishi na mtoto huyo, baada ya wanandoa hao kutengana.

Alisema mtuhumiwa inasemekana alimchukua kwa nguvu mtoto huyo kutoka kwa mama yake na kwenda naye nyumbani kwake kisha kumuua na kumfukia sebuleni ndani ya nyumba yake.

Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya shughuli za maziko.

Hata hivyo, Kamanda Diwani alisema kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo zinafanyika, huku akiwataka wanandoa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

chanzo:mtanzania
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment