MAKUNDI YA WANAWAKE WAPIGANAJI KATIKA MAKUNDI YA WAASI NCHINI CONGO

Kanali Fanette Umuraza akiwa katika makao makuu ya M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Kongo. Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka32 na mwenye shahada ya chuo kikuu katika sayansi ya siasa, anaongoza kwa umakini mkubwa aidolojia ya kiongozi wa kijeshi wa M23, Sultani Makenga.


Meja wa M23 Fanette Rwagati, akicheza pamoja na wanawake katika mji wa  Kibumba.


Meja wa M23 Fanette Rwagati


Kanali Fanette Umuraza, ana umri wa miaka 32. Fanette alijiunga na M23 baada ya kushiriki mapigano katika kundi la waasi la CNDP, watangulizi wa M23. Anasema kuwa aliyachagua makundi haya ya waasi kwa sababu yana mawazo na itikadi kama zake. Hapa M23 wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia migawanyiko ndani ya kundi hilo, katika eneo la Kibumba, Kivu Kaskazini, ambalo liliwahi kudhibitiwa na kundi la M23.


Umuraza anasema kuwa anataka kuwakomboa wanawake wa Kongo dhidi ya vitendo vya ubakaji na unyanyasaji. Hata hivyo, makundi ya waasi yamekuwa yakishutumiwa kufanya vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake.


Tangu mwaka 2012, Meja Mathilde Samba amekuwa akitumikia kundi la M23 akiwa bega kwa began a mumewe.


Akiwa na umri wa miaka 31, Meja Mathilde Samba (kulia) tayari ana uzoefu mkubwa wa kijeshi. Baada ya kulitumikia jeshi la serikali ya Kongo kwa muda wa miaka 13, alijiondoa jeshini Novemba 2012 na kujiunga na M23. Hapa anaonekana akiwa na mumewe, Kanali Jean-Marie Labila, mwenye umri wa miaka 49.


Meja Mathilde Samba (31) katika gwaride la polisi ya M23. Mathilde alikuwa katika jeshi la serikali kwa zaidi ya miaka 10. Aliondoka jeshini Novemba 2012, akajiunga na M23 pamoja na mumewe na kuwasafirisha watoto wake kwenda mjini Kinshasa. Hapa akiwa katika kambi ya M23, eneo la Rutshuru, Kivu ya Kaskazini, ambalo lilikuwa likidhibitiwa na waasi wa M23.

Tangu mwaka 2012, Meja Mathilde Samba amekuwa akitumikia kundi la M23 akiwa bega kwa began a mumewe.


Hapa Meja Mathilde Samba akiwa katika kambi ya M23, eneo la Rutshuru, Kivu ya Kaskazini, ambalo lilikuwa likidhibitiwa na waasi wa M23.

Marimakile Kiakimuakisubua alishuhudia familia yake ikiuawa. Akiwa amejiunga na kundi la Mai Mai Shetani, ana matumaini ya kulipa kisasi.


Wapiganaji wa kike wa kundi la waasi la Mai Mai Shetani wakifanya doria kwenye mashamba huko Kivu. Wanaitwa Mai Mai (Maji Maji) kwa sababu hufanyiwa matambiko kwa kutumia “maji matakatifu” yanayowafanya wasionekane.







Kutoka kushoto: Kapteni Liliane Katiwa, Luteni Marimakile Kiakimuakisubua, Meja  Francine Kanier, Luteni Kanieremervè Uivin, mwenye umri wa miaka 16, Luteni  Rehema Rahijya, wakiwa kwenye kambi ya Mai Mai Shetani/FPD, Nyamilima, Kivu Kaskazini, nchini Kongo.

Mai Mai Shetani/FDP, kambi ya Buramba, Nyamilima, Kivu kaskazini Kivu, DRC
Ingawa idadi kamili ya wapiganaji wa kike katika makundi ya waasi haijulikani, ni dhahiri kuwa hawajiungi na makundi hayo kwa hiari. Mara nyingi, wanawake na mabinti hujiunga na makundi hayo baada ya kutekwa.


Mai Mai - Shetani

Luteni Rehema Rahijya hajui tarehe yake ya kuzaliwa. Hapa anaumwa Malaria, lakini hatumii dawa yoyote. Alizaliwa eneo la Nyamilima. Alijiunga na Mai Mai Shetani/FDP mwaka mmoja uliopita baada ya watu wenye silaha kuishambulia familia yake: walimbaka dada yake na kuiba mifugo. Hataki kuolewa na anadhani kuwa hapo baadaye hatapata kazi kwa sababu ni muasi. Hapa ni katika kambi ya kijeshi ya Buramba, Nyamilima, Kivu Kaskazini, DRC.


Kanieremervè Uivin, mwenye umri wa miaka 16, ndiye binti mkubwa katika familia yake. Baba yake aliuawa na kundi pinzani miaka kadhaa iliyopita, na shangazi yake alibakwa, jambo lililomsukuma Uivin kujiunga na waasi wa Mai Mai Shetani. Ana ndoto za kurudi shule na kumalizia masomo yake.



Liliane Katiwa, akiwa katika kambi ya kijeshi ya Buramba, ana ndoto za kurudi katika maisha ya kawaida na kuwa na kazi ya kawaida pia.










PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUMS
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment