TUKIO LA KUJERUHIWA KWA UFOO SARO

 


Asubuhi ya leo, mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, Ufoo Saro alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari (sio Mzizima 24), Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kamanda Wambura, alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya asubuhi ya leo.

Kamanda Wambura alidai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan, ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikuwa na ugomvi baina ya wawili hao na waliposhindwa kuelewana waliamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro (mama mkwe) ili awasuluhishe.

Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa mwanaume ndiye mwenye matatizo, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanaye na ndipo alipotoa bastola na kumpiga risasi ya kichwa mama wa Ufoo Saro na kumuua papo hapo.

Alipomuua mama, alimpiga Ufoo Saro risasi mbili, tumboni na mguuni na kudhani kuwa amemuua na kisha akajipiga risasi mwenye kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.



TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZA TUKIO HILI…  TUNAHITAJI MAONI YAKO KUHUSU HUDUMA ZETU.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment