KOCHA aliyetupiwa virago mwishoni mwa msimu, Mfaransa
Patrick Liewig amewasili nchini kwa ajili ya kuja kudai fedha zake, dola za
Kimarekani 18,000 za malimbikizo ya mishahara yake akiwa kazini katika klabu
hiyo tangu Januari hadi Mei, mwaka huu.
Liewig amelenga mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga
ambayo huwa na mapato mengi na amefikia katika hoteli ya Sapphire Court,
Kariakoo, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini, Liewig amesema
kwamba amefuata fedha zake na tayari ameanza kumtafuta Mwenyekiti wa Simba SC,
Alhaj Isamil Aden Rage ili wamalizane.
“Siwezi kuzungumza mengi kwa sasa hadi nitakapokutana na
viongozi wa Simba SC, ila nawadai dola 18,000 pamoja na nyongeza ya tiketi ya
ndege kwenda na kurudi dola 1, 800,”alisema.
Juni 20, mwaka huu Simba SC ilimlipa Liewig jana dola za
Kimarekani 10,000 kati ya dola 26,000 alizokuwa anadai klabu hiyo baada ya
kumvunjia Mkataba na kuahidi kumlipa kiasi kilichobaki mwezi huu.
Liewig alikuwa anadai malimbikizo ya mishahara ya miezi
miwili, dola 12,000 na akalipwa dola 12,000 za kuvunjiwa Mkataba wakati dola
2,000 ni za tiketi yake ya kurejea kwake.
Kocha huyo alivunjiwa Mkataba wakati amepwa likizo ya
kwenda mapumzikoni kwao, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake amepewa Alhaj Abdallah Athumani Seif
‘King Kibadeni’.
Hata hivyo, baada ya kurejea nchini alifanya mazungumzo
na uongozi wa Simba, hatimaye wakakubaliana kulipana kwa awamu, fungu la mwisho
likitarajiwa kutolewa mwezi huu.
Liewig alisani Mkataba wa mwaka mmoja na nusu Januari
mwaka huu kuifundisha Simba SC akirithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan
Cirkovick aliyetupiwa virago.
Katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo kwa miezi
mitano, Liewig aliiongoza Simba katika mechi 25 akiiwezesha kushinda tisa, sare
nane na kufungwa saba.
CHANZO: Dina Ismail Blog
0 comments:
Post a Comment