TETEMEKO LA ARDHI LAITIKISA TENA INDONESIA





Tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcha 7.2 kimelikumbuka eneo la mashariki mwa Indonesia.

Tetemeko hilo kubwa lilipiga katika eneo lenye milima la nchi hiyo katika jimbo la Papua Magharibi leo Jumamosi, lakini hakujaripotiwa vifo au hasara ya moja kwa moja.

Kwa mujibu wa idara ya Jiolojia ya Marekani, tetemeko hilo lilitokea kilometa 256 (maili 159) mashariki ya Enarotali na kina chake kilikuwa kilometa 58 (maili 36) chini ya ardhi.

Kituo cha Tahadhari ya Tsunami cha Pacific (The Pacific Tsunami Warning Center) mjini Hawaii kilisema kuwa hapakutokea tsunami yoyote. Wakaazi walizikimbia nyumba zao wakiwa na kihoro, na wengi waliendelea kubaki nje wakihofia maisha yao.

Indonesia ni eneo linalokumbwa sana na matetemeko ya Ardhi kwa kuwa ipo kwenye eneo lijulikanalo kitaalamu kama Pacific Ring of Fire, ambalo ni maarufu kwa  harakati nyingi za matetemeko na volcano.

Mwaka 2004 tetemeko zito lililopiga nje ya pwani ya Indonesia lijulikanalo kama Tsunami liliua watu 230,000 katika nchi 13 zinazopakana na Bahari ya Hindi. Vifo vingi vilitokea katika jimbo la kaskazini la Aceh nchini Indonesia.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment