SERIKALI IBEBE GHARAMA ZA USAFIRISHAJI, IPUNGUZE KODI ZA USAFIRISHAJI KWA MASLAHI YA WATANZANIA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 05/04/2013
Mhariri
SERIKALI IBEBE GHARAMA ZA USAFIRISHAJI, IPUNGUZE KODI ZA USAFIRISHAJI KWA MASLAHI YA WATANZANIA.
CUF- Chama cha Wananchi, tunashangazwa sana na tendo la Sumatra kutangaza kupandisha nauli za usafiri Inchi nzima. Sumatra wanapaswa kutambua kwamba, unapopandisha Nauli , maana yake umepandisha Gharama za Maisha kwa Watanzania wote. Kwa hoja ya Sumatra kuhusu ombi la Wanyabiashara za Usafirishaji Nchini, Sumatra inapaswa kuishauri Serikali kubeba Mzigo huo, kwa kupunguza kodi mbali mbali zinazotozwa ili kuweza kumsaidia Mwananchi wa kawaida.
Tanzania ni Nchi yenye watu wengi wasio na Ajira. Watanzania waliowengi wanaishi kwa kutegemea Kilimo, lakini hata Mkulima wa Mbozi anategemea Mnunuzi wa Mazao yake atoke Mwanza na maeneo mengine ili aweze kwenda kununua Mazao yake, Mtu anae athirika zaidi na Tamko la SUMATRA ni Mtanzani wa Vijijini ambae maisha yake yote kwa kila anachokitumia ,kina hitaji usafiri. Huwezi kupandisha gharama za usafiri kwa Abiria huku ukidhani kwamba , gharama za Mizigo na bidhaa zingine zitabaki kuwa kama zilivyo.
CUF – Chama cha Wananchi, kinaona wakati umefika sasa, kwa Serikali na Mamlaka zake kujifunga Mikanda na kubeba Mzigo kwa niaba ya Wananchi ili kuweza kutoa nafuu kwa Wananchi. Wananchi wamefun ga Mikanda vya kutosha, sasa ni vyema na ni busara kwa SUMATRA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu Ombi la Wafanyabiashara hao, na kisha kuishauri Serikali iweze kupunguza kodi ili kufidia gharama za uendeshaji kwa Wafanyabiashara wa shughuli za Usafirishaji hapa Tanzania.
Ukiachna na bei za Mikoani kwa watu wazima, tutazame suala la Nauli ya Mwanafunzi kuwa TSHS 200/= , maana yake Familia yenye watoto 5 kuanzia Shule ya Msingi mpaka Sekondari, wanaotumia Mabasi mawili kwa siku, Baba au Mama atahitaji kuwa Jumla ya TSHS 2,000= kwa siku na kwa mwezi ni 60,000/= Nje ya Gharama za Mzazi mwenyewe. Gharama hizi kubwa kwa Mwananchi wa kawaida ndio maana CUF-Chama cha Wananchi tunaishauri SUMATRA kulitazama upya jambo hili, na baadae kutoa ushauri utokua na Manufaa kwa pande zote mbili, kwa maana ya Wafanyabiashara na Wananchi.
CUF-Chama cha Wananchi kinatoa wito kwa SUMATRA kulitazama jambo hili kwa umakini na kwa misingi ya kuimarisha uchumi wa Wananchi waliowengi zaidi. Endapo SUMATRA wataendelea kuishauri vibaya Serikali, katika jambo hili , basi CUF-Chama cha Wananchi tutajipanga kuchukua hatua za kisiasa Nchi nzima kwa lengo la kuwatetea Wanyonge wa Nchi hii.
Imetolewa na
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari Haki za Binadamu na Mahusiano ya Umma CUF .
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment