AINA MPYA YA MAFUA YA NDEGE YASITISHA BIASHARA YA KUKU NCHINI CHINA




Chickens are seen in a farm in Zouping, east China 


China imefunga masoko ya kuku mjini Shanghai baada ya kuku wengi kuzidi kuteketezwa ili kuzua usambaaji wa virusi vipya vya mafua ya ndege.

Masoko ya kuku katika mji wa Shanghai yalifungwa baada ya mamlaka kupiga marufuku biashara hiyo ili kuzuia kusambaa kwa mafua ya ndege aina ya H7N9 ambayo mpaka sasa yamegharimu maisha ya watu sita.

Vyombo vya habari za serikali viliripoti kuwa siku ya Ijumaa mamlaka za China ziligundua dalili za virusi vipya vya mafua ya ndege katika maeneo mengi ya mji wa Shanghai baada ya kuchinja kuku zaidi ya 20,000 kwenye soko kuu la kuu la mji huo.

"Biashara imesitishwa kwa sababu ya mafua ya ndege. Muuzaji amerudi nyumbani kwa sababu hana cha kufanya," alisema mchuuzi mmoja wa samaki.

"Watu wana wasiwasi," alisema Yan Zhicheng, meneja mstaafu wa kiwanda ambaye kama wazee wengine wa mji wa Shanghai ambao hufanya safari za kila siku katika soko hilo. "Watu wa Shanghai hutumia sana bata na kuku kwa wingi. Sasa hivi hawawezi kuwagusa."

China imethibitisha kadhia 16 za ugonjwa huo mpya tangu ulipogunduliwa wiki moja ilipopita.  

Virusi vya H7N9 ni aina ya mafua ya ndege ambayo hayakuwahi kuonekana kwa mwanadamu hapo kabla.


Mamlaka za China zinashikilia kuwa hakuna ushahidi kwa ugonjwa huo kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment