SYRIA: KIONGOZI WA MUUNGANO WA UPINZANI AJIUZULU

Ahmed Moaz Al-Khatib


Kiongozi wa Muungano wa Kitaifa wa Syria, Ahmed Moaz Khatib ametangaza kujiuzulu wadhifa wake miezi minne tu baada ya kuchaguliwa.

Kiongozi huyo wa kundi la Upinzani linaloungwa mkono na mataifa ya Magharibi amejiuzulu kutokana na migongano iliyopo ndani ya muungano huo. Katika taarifa yake alisema kuwa anajiuzulu “ili kuweza kufanya kazi kwa uhuru ambao haupatikani ndani ya taasisi rasmi.”
Muungano huo umekuwa ukikabiliwa na migogoro ya ndani kwa ndani. Hivi karibuni wamekuwa wakifanya jitihada za kuunda serikali ya mpito, ambayo itatumika kama mabadala wa serikali ya sasa ya Rais Bashar Assad iwapo ataondolewa au kujiuzulu.

TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment