JAMHURI YA AFRIKA YA KATI: IKULU YAANGUKIA MIKONONI MWA WAASI




Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanasema wameitwaa ikulu ya rais katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, baada ya mapambano mazito.

"Tumeichukua ikulu. [Rais Francois] Bozize hakuwepo," alisema mmoja wa makamanda wa waasi, Kanali Djouma Narkoyo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Alisema kuwa waaasi walikuwa wakipanga kuelekea kwenye kituo cha redio ya taifa, ambapo kiongozi wa waasi hao Michel Djotodia anapanga kuzungumza.

Maafisa wa serikali walithibitisha kuwa Bozize alikimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. "Waasi wameudhibiti mji," msemaji wa rais, Gaston Mackouzangba, alisema na kuongeza, "ninatarajia hapatakuwa na ulipizaji kisasi wowote."

Waasi wa Seleka walianzisha upya mapigano wiki hii katika hiyo iliyowahi kuwa koloni la Ufaransa, wakiapa kumuangusha Bozize, ambaye wanamtuhumu kwenda kinyume na mkataba wa amani uliosainiwa mwezi Januari uliokusudiwa kuwaingiza wapinaji wa waasi katika jeshi la taifa.

Mwaka jana kundi hilo lilianzisha mapambano na serikali ya rais Bozize na kukaribia kuutwaa mji mkuu wakimtuhumu rais huyo kushidnwa kuheshimu makubaliano ya awali ya kuwapa wapiganaji hao pesa na kazi ili waweke silaha zao chini.

'HAKUNA KITISHO CHA MOJA KWA MOJA'

Hizi ni ghasia mpya kabisa katika mlolongo wa mapigano,mapambano na mapinduzi ya waasi yaliyolikumba taifa hilo la katikati mwa Afrika tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.

Ufaransa ambayo ilikuwa na wanajeshi wapatao 250 katika nchi hiyo, ilituma askari wengine 150 kwa ajili ya kuulinda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bangui, kilisema chanzo kimoja cha kidiplomasia.

"Tumewataka raia wetu wabaki nchini. Kwa sasa hakuna wasiwasi tena,” kilisema chanzo hicho. “Kwa sasa hakuna kitisho cha moja kwa moja kwa raia wetu.”

Uwanja huo wa ndege ulio jirani na kitovu cha mji, ni njia muhimu ya kutokea kwa raia 1200 wa Ufaransa wanaoishi katika nchi hiyo, hususan mji mkuu Bangui.

Afrika ya Kusini ilituma wanajeshi 400 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa jeshi la serikali ya Bozize, na kuungana na mamia ya walinda amani kutoa Jumuia ya ukanda wa Afrika ya Kati. Walinda amani hao walipambana bega kwa began a jeshi la serikali dhidi ya waasi.

Siku ya ijumaa, redio ya taifa ilikuwa imetangaza kuwa Afrika ya Kusini ingeongeza wanajeshi baada ya Bozize kukutana na Rais Jacob Zuma mjini Pretoria.

CHANZO: ALJAZEERA NA MASHIRIKA YA HABARI

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment