PAC yaishauri Serikali namna ya kuinusuru kampuni ya TTCL

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.

  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. 

PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015. Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. 

PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment