Rais wa zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, aliyemaliza
muhula wake wa uongozi mwaka jana anaripotiwa kurudi kwenye taaluma yake ya
ufundishaji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Serbia News, inasemekana Rais
huyo aliyekuwa mashuhuri wa misimamo yake husafiri katika basi la abiria
kuelekea kazini kwake ambapo anafundisha kwenye Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia. Ahmadinejad ana shahada ya uzamivu – Ph.D- ya uhandisi.
0 comments:
Post a Comment