Luis Suarez |
Aliyekuwa
beki wa timu ya taifa ya Uruguay Gus Poyet, amembashiria mema mshambuliaji wa
klabu ya Liverpool Luis Suarez, kwa kusema huenda akang’ara katika fainali za
kombe la dunia na mwishowe kutangazwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizo.
Gus
Poyet, ambae kwa sasa ni meneja wa klabu ya Sunderland ya nchini Uingereza
amesema uwezo unaoendelea kuonyesha na mshambuliaji huyo kwenye ligi ya nchini
humo, ameanza kuhisi huenda akaona mengi zaidi kutoka kwa Luis Suarez
atakapokua na timu ya taifa ya Uruguay wakati wa fainali za kombe la dunia.
Poyet
amesema kila kukicha Luis Suarez amekua na mambo muhimu anayo yaonyesha
anapokua uwanjani, kwa kuisaidia klabu yake ya Liverpool ambayo imeanza
kufikiriwa huenda ikaibuka kidedea kwenye ligi ya nchini Uingereza msimu huu.
Amesema
tangu msimu huu ulipoanza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekua
akionyesha kiwango kizuri hali ambayo anaamini itaendelea kumsaidia katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia ambazo zinasubiriwa
kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ulimwenguni kote.
“Luis
Suarez ni mshambuliaji ambae mara nyingi amekua akiwapa shida wapinznai wake na
wakati mwingine naamini mabeki huchukia pale wanapomuona yupo kwenye kikosi cha
klabu yake ya Liverpool” Alisema Gus Poyet ambae alichezea timu ya taifa ya
Uruguay katika michezo 26 na kuwa kuwa mmoja wa wachezaji walioiwezesha timu
hiyo kutwaa ubingwa wa Copa America mwaka 1995.
Wakati
huo huo Gus Poyet ameonyesha kuwa na imani kubwa na timu ya taifa ya Uruguay
ambapo ameitabiria kuwa moja ya timu ambazo huenda zikatwaa ubingwa katika
fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Poyet
amesema hatua ya kumaliza katika nafasi ya nne katika fainali za kombe la dunia
za mwaka 2010, iliwapa morari ya hali ya juu wachezaji wa timu hiyo, hivyo ana
hakika hakuna kitakacho shindikana katika fainali za mwaka huu.
Pia
gwuiji huyo wa klabu za Chelsea pamoja na Newcastle Utd za nchini Uingereza
akatumia kigezo cha timu ya taifa lake kutwaa ubingwa wa Copa America, mwaka
2011 kuwa sehemu ya kuipa nafasi kubwa Uruguay kufikia malengo ya kutwaa
ubingwa wa dunia.
“Kwa
Mafanikio waliyofikia wachezaji wa timu ya taifa ya Uruguay katika kipindi cha
miaka minne iliyopita, sina budi kuamini mwaka huu, huenda mambo yakawa mazuri
katika fainali za kombe la dunia” Gus Poyet aliweka bayana.
Timu
ya taifa ya Uruguay ambayo imepangwa katika kundi la nne itaanza kampeni ya
kuwania ubingwa wa dunia kwa kucheza na timu ya taifa ya Costa Rica, kisha
mchezo wa pili itapambana na timu ya taifa ya Uingereza kabla ya kumaliza na
mabingwa wa dunia wa mwaka 2006 timu ya taifa ya Italia.
0 comments:
Post a Comment