Radamel Falcao |
Mshambuliaji
kutoka nchini Colombia Radamel Falcao, amesema yupo tayari kuhatarisha maisha
yake ya soka, ili mradi acheze fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo
zitafanyika nchini Brazil kuanzia Juni 12 hadi Julai 13.
Radamel
Falcao, ameonyesha kuwa tayari kufanya hivyo kutokana na kuendelea kuuguza goti
la mguu wake wa kulia, ambapo inadaiwa huenda akazikosa fainali hizo kutokana
na jeraha kubwa linalomkabili kwa sasa.
Falcao
ambae ni mshambuliaji wa klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa amesema atafanya
kila njia ili aweze kukamilisha azma yake ya kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya
taifa ya Colombia ambacho kitashiriki fainali hizo.
Amesema
ni vigumu kwake kuamini kama atazikosa fainali hizo, kwa kisingizio cha kuwa
majeruhi, hali ambayo anaamini inaweza kurekebishwa kwa gharama zozote ambazo
amedai yupo tayari kuzotoa mfukoni mwake.
"Ni
wazi kwamba kila mmoja anafahamu namna nilivyo shirikiana na wenzangu kwa ajili
ya kutafuta nafasi ili tushiriki fainali za kombe la dunia, hivyo nipo tayari
kwa lolote ili niwe sehemu ya kikosi kitakacho malizia kazi nchini Brazil”
Alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
"Siwezi
kuacha ndoto zangu zikayeyuka tena kwa kuliona taifa langu la Colombia
likiangamia ama kupata mafanikio nchini Brazil, bila ya mimi kuwepo hilo
halitokua jambo jema kwangu” Aliongeza Falcao.
Radamel
Falcao, aliumia goti la mguu wake wa kulia mwezi januari mwaka huu wakati klabu
yake ya AS Monaco ilipokua ikikabiliwa na mchezo wa kuwani kombe la nchini Ufaransa
dhidi ya Chasselay.
Mpaka
anapatwa na majereha ya goti Falcao alikua ameshaifungia AS Monaco mabao tisa
katika michezo 17 aliyocheza, na kwa upande wa timu ya taifa ya Colombia
mshamnbuliaji huyo ameshacheza michezo 51 na kufanikiwa kufunga mabao 20.
Katika
fainali za kombe la dunia timu ya Colombia imepangwa katika kundi la tatu
sambamba na Ivory Coast, Japan pamoja na Ugiriki.
0 comments:
Post a Comment