Shirikisho
la soka nchini Italia FIGC limetangaza msimamo wa kuwa na imani na kocha mkuu
wa timu ya taifa ya nchi hiyo Cesare Prandelli, ambae ana jukumu la kuiongoza
The Azzuri kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.
Raisi
wa shirikisho hilo Giancarlo Abete amesema uwezo wa kocha huyo bado ni kubwa,
na wana hakika utakua chachu kwa timu yao kufanya vyema kwenye fainali hizo,
licha ya baadhi ya wadau wa soka nchini Italia kuanza kumkejeli.
Giancarlo
Abete, amesema kwa kuonyesha ni vipi walivyokua na imani kubwa na Cesare
Prandelli, tayari wameshampa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu ya taifa
ya Italia hadi mwaka 2016 ambao utaanza kufanya kazi mara baada ya mkataba wa
sasa utakaofikia kikomo kwa mwezi July mwaka huu.
Kiongozi
huyo wa soka nchini Italia amesisitiza kwamba pamoja na kebehi kuelekezwa kwa Cesare
Prandelli, wameamua kumpa mkataba mpya kwa makusudi huku wakiamini hata kama
atashindwa kufanya vyema katika fainali za kombe la dunia, bado atakua na
nafasi nyingine ya kujipanga kwa ajili ya fainali za mataifa ya barani Ulaya za
mwaka 2016.
“Tunajua
ni nini tunachokifanya kwa maslahi ya soka la nchini Italia, hatuwezi
kuwasilikiza baadhi ya watu kwa kuamini uwezo wa Cesare Prandelli, umeshuka
bali tunaamini katika utendaji wa kazi ambapo kwa kocha huyu tunaridhishwa na
uwezo wake” Alisema Giancarlo Abete.
Katika
hatua nyingine Giancarlo Abete, amewataka baadhi ya wadau wa soka nchini Italia
wanaopinga uwezo wa Prandelli, kwa kukumbuka namna alivyoichukua timu ya taifa
ya Italia mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, na kuifikia
mafanikio ya kuifikisha timu hiyo katika hatua ya fainali kwenye michuano ya
barani Ulaya ya mwaka 2012.
Wadau
wa soka nchini Italia wamekua wakihoji uwezo wa kocha huyo mwenye umri wa miaka
56 kutokana na kushindwa kuiwezesha Italia kutwaa ubingwa wa barani Ulaya, kwa
kuruhusu timu hiyo kufungwa idadi kubwa ya mabao kwenye mchezo wa hatua ya
fainali dhidi ya Hispania.
Wasi
wasi mwingine kwa wadau hao unatokana na muonekanano wa kundi la nne katika
fainali za kombe la dunia ambapo Italia imepangwa katika kundi hilo na timu za Uruguay,
Uingereza pamoja na Costa Rica.
0 comments:
Post a Comment