Arjen Robben |
Mshambuliaji
kutoka nchini Uhonazo Arjen Robben amesema katu
hawaidharau timu ya Man utd ambayo wanakutana nayo hii leo katika mchzo wa
hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Arjen Robben amesema wanatambua FC Bayern Munich wanapewa nafasi
kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo, kutokana na udhaifu wa wapinzani
wao, lakini wao kama wachezaji wa The Bavarians wanatambua mchezo wa soka haupo
hivyo kama wengi wanavyofikiria.
Robben amesema wanawaheshimu Man Utd, kutokana na kuwa na historia
nzuri katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya, hivyo watacheza kwa kujituma
wakati wote huku wakitambua lolote laweza kutokea ndani ya dakika 90.
"Katika soka
unahitaji kumuheshimu kila unaekutana nae na sisi kama FC Bayern Munich japo
tunapewa nafasi kubwa ya kushinda, bado tunaamini lolote laweza kutokea ndani
ya dakika 90, hivyo hata mashabiki wanatashili kuwa na subra” Alisema Robben.
"Tunakwenda Old
Trafford huku tukianimi tunapewa nafasi kubwa ya kushinda lakini kila mmoja
anaejua maana ya soka anapaswa kutambua hatua ya robo fainali tuliyofikia ipo
wazi kwa kila mmoja kusonge mbele” Aliongeza mshambuliaji huyo mweny umri wa
miaka 31.
FC Bayern Munich hii leo
wanarejea kwa mara ya pili mjini Manchester katika msimu huu, baada ya kupangwa
na Man city kwenye hatua ya makundi, ambapo walipocheza mchezo wa hatua hiyo
mjini humo walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja.
Mchezo mwingine ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo
fainali utachezwa nchini Hispania ambapo FC Barcelona watakua nyumbani
wakipambana na Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment