Afisa utetezi wa haki za kiuchumi wa OXFAM Mkamiti Mgawe
akielezea kwa kina namna ambavyo wanafanya mchujo wa kumpata mshiriki wa awali wa mama shujaa
wa chakula/ Maisha Plus ambapo washiriki wanatarajia kuingia katika kijiji cha
Maisha Plus mwezi wa tatu mwaka huu
2014.
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa
Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo
unavyo fanyika ili kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha
Plus/Mama shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale
watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
|
Majaji wakuu walioteuliwa kwa ajili ya kufanya mchujo wa
kuchagua Mama Shujaa wa Chakula 30 na vijana 45 ambao baadae watafanyiwa
usahili na kubakiza wanawake 20 pamoja na vijana 30 kutoka Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi.
|
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa
Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) aliyevaa kofia akipitia kwa umakini
Fomu za mchujo za Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus.
|
Wanafunzi 17 ambao wana fani mbalimbali na waliojitolea
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Tumaini ambao
wanawasaidia majaji kupitia fomu za mchujo ili kuwapata wale watakaofanikiwa
kuingia katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
|
Baadhi ya wanachuo wakiwa wanaendelea kupitia Fomu kwa
umakini kuhakikisha wanawatendea haki washiriki wote walioleta Fomu zao.
|
Mmoja wa wanachuo akifanya maheesabu kwa makini ili
kutoa alama kwa washiriki walioleta fomu kwa ajili ya mchujo ya kuwapata
watakaoingia katika usahili wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula.
|
Baadhi ya Fomu zikiwa zimemalizika kupitiwa na wanafunzi
wa Chuo kikuu ili kupelekwa kwa Majaji wakuu.
|
SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA/ MAISHA PLUS
* Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus
zakusanywa
* Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake
20 na vijana 45
Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa
wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo
ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki.
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam
akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema zoezi la kupitia fomu
litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi Alhamisi tarehe 6 Februari
2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000
ambazo tumekishwazipokea na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali
za nchi yetu. Baada ya uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja
na vijana 45 ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia
kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kitengo cha Jinsia. “
Jopo la majaji linajumuisha waliobobea kwenye masuala
yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi,
biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii.
Majaji ni kama
wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la
VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma
mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ; Francis Bonda
Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund
Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki wa shindano la
Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka
shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa
thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto,
Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012.
Washiriki wa
Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya,
Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni
25.
(Kwa hisani ya Nkoromo blog)
0 comments:
Post a Comment